Shindano la Ubunifu wa Mifumo ya Tehama (Hackathon)

Shindano la Ubunifu wa Mifumo ya Tehama (Hackathon)

Matumizi ya Tehama katika kutatua baadhi ya changamoto za Jiji la Mwanza

Katika juhudi zake za kukuza ubunifu na kukabiliana na changamoto mbali mbali nchini, Tume ya Taifa ya Sayansi (COSTECH) kwa kushirikiana na Atamizi yake ya DTBi, imeandaa mpango wa kuibua vipaji vya ubunifu katika Tehama kwa kutumia vijana wabunifu kutoka mkoani Mwanza kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza na Jiji la Mwanza.